| (Kiswahili Version) Justus Bahati Wanzala | ||
| Kalimani wa Shirika la ISN wa Lugha ya Kiswahili. | ||
| ||
| "Mara ya kwanza niliposoma kuhusu huu ugonjwa scleroderma, niliguswa na moyo wa huruma ndipo nikaamua kusaidia karidi ya uwezo wangu katika kukabiliana nao." | ||
Jina langu ni Justus Bahati Wanzala, na mimi ndiyo kalimani wa Shirika la ISN wa lugha ya Kiswahili. Ninahudumu kama mwandishi wa habari na pia nina tafsiri habari kutoka lugha ya Kiingereza hadi Kiswahili katika Shirika la Kitaifa la Utangazaji Nchini Kenya, KBC. Nilifuzu kama mwandishi wa habari kwenye chuo cha Kitaifa cha Uwandishi wa Habari, Nchini Kenya, KIMC, jijini Nairobi. Kwa wakati huu ninafanya kazi kama mwandishi wa habari na tena kama kalimani na mara ya kwanza niliposoma kuhusu huu ugonjwa wa scleroderma, niliguswa na moyo wa huruma ndipo nikaamua kusaidia karidi ya uwezo wangu katika kukabiliana nao. Nina fahari kubwa kuwa niko mmojawapo wa wale wanaozambaza habari kuhusu maradhi haya katika lugha yangu ya kitaifa ya Kiswahili, kupitia kwa huduma ninayotoa kwa shirika la ISN. Unaweza kuwasiliana nami katika lugha ya Kiingereza au Kiswahili kwa njia ya mtandao. |
